Mshahara! Kuna jambo litasemwa

ARUSHA: Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amewaondoa hofu wafanyakazi nchini kuhusu ongezeko la mishahara na kuwapa tumaini kuwa hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan atasema jambo.

Akizungumza leo katika Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yanayofanyika kitaifa mkoani Arusha Dk Mpango amesema licha ya changamoto zinazoikumba dunia na kuathiri mifumo mbalimbali, Taifa linajivunia uchumi stahimilivu.

“Tathimini ya Serikali na taasisi za kimataifa zimeonesha kuwa uchumi wa taifa umekuwa stahimilifu kwa kiwango cha kuridhisha, hivyo Mama wa Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan amenituma niwaambie wafanyakazi kama mambo yakiendelea hivi atasema jambo hivi karibuni”, amesema Dk Mpango.

Dk Mpango ametoa wito kwa wafanyakazi nchini kuendelea kuchapa kazi kwa maslahi ya taifa kwa kutanguliza uzalendo.

Habari Zifananazo

Back to top button