KLABU ya Yanga, imemsajili kiungo wa zamani wa Azam FC, Mudathir Yahya kwa mkataba wa miaka miwili.
Mudathir amejiunga na Yanga akiwa mchezaji huru, baada ya mkataba wake na waajiri wake wa zamani Azam FC kumalizika tangu mwishoni mwa msimu uliopita.