Muhimbili yafanya upasuaji wa bandama
Ni Kwa mara ya kwanza
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imefanya upasuaji mkubwa wa kuondoa bandama lenye shida kwa mgonjwa kwa njia ya matundu madogo (laparoscopic splenectomy).
Upasuaji huu ni wa kwanza kufanyika hapa nchini ambao umefanywa na madaktari wa upasuaji wa MNH kutokana na ubobezi walionao.
Akizungumza na HabariLEO, Daktari bingwa wa upasuaji mfumo wa chakula na ini ambae aliongoza jopo la madaktari, wauguzi, na wataalamu wa ganzi na usingizi katika upasuaji huo, Dk
Kitembo Kibwana amesema, upasuaji huo umekua na mafanikio makubwa.
Akifafanua amesema, “Bandama (wengu) ni kiungo cha mwili chenye nafasi katika mzunguko wa damu. Lipo ndani ya fumbatio ya mwili karibu na mfuko wa chakula ambapo kazi yake kubwa ni kuongeza seli nyeupe za damu na kuondoa seli nyekundu za damu zilizozeeka.
“Amesema
Amesema, kwa watoto bandana lina jukumu la kutengeneza seli nyekundu za damu. Watu wazima kwa kawaida wanaweza kuishi bila ya bandama.
Aidha, amesema hospitali ya Taifa Muhimbili inaendelea kuboresha huduma zake mbalimbali ikiwemo upasuaji mkubwa, uchunguzi na mifumo ya utoaji huduma kwa ujumla wake.