Mwanahabari apitishwa udiwani Handeni

HANDENI : CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Handeni mkoani Tanga kimetangaza majina ya wagombea udiwani. Mwandishi wa habari na mdau wa maendeleo wilayani humo, Kambi Mbwana amepitishwa kugombea nafasi hiyo ya udiwani katika Kata ya Kwamatuku.
Katika mchakato wa kura za maoni zilizofanyika Agosti 4, mwaka huu Mbwana aliibuka na ushindi kwa kupata kura 439. Mpinzani wake, Mustafa Beleko aliyekuwa anawania nafasi hiyo kwa kipindi cha nne, alipata kura 207 na mshindi wa tatu Joseph Minango amepata kura saba.
Vikao vya mwisho vya uteuzi katika ngazi ya mikoa kwa madiwani vilikamilika Agosti 13 mwaka huu tayari kwa wagombea hao kuwania nafasi hizo katika Uchaguzi Mkuu. Baada ya kupata taarifa za kupitishwa kuwa mgombea wa udiwani wa kata hiyo. SOMA: Vipaumbele 10 vya CHAUMMA kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mbwana alisema, “Namshukuru Mungu jina langu limepenya mbele ya vikao vya uteuzi. Zilikuwa ni siku ngumu tangu tulipochukua fomu, tulivyochujwa na baadaye kufikishwa kwa wajumbe na hatimae kupata kura nyingi za wenye chama chao



