Mwanasiasa nguli ampigia debe Rais Dk. Samia

DAR-ES-SALAAM: MWANASIASA nguli nchini, Balozi Dkt. Getrude Mongella amewataka wanawake wa Tanzania kuungana na kumpigia kura mwanamke katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ili kutimiza malengo ya maazimio ya mkutano wa Beijing yaliyosisitiza ongezeko la idadi ya viongozi wanawake.

“Safari hii tuonyeshe kwamba mwanamke anachagulika, kama unayo ya kwako weka rohoni, lakini ajenda yetu iwe kumchagua mwanamke,” alisema Balozi Dkt. Mongella.

Aliongezea, “Mimi naenda Marekani kifua mbele na yule baba, nataka kumwambia tunamuweka mwanamke. Tukiwa na nia, sisi wanawake wa Tanzania tunakwenda kushirikiana na serikali ili tuondokane na dimbwi la kuombaomba.” Alimalizia Dkt. Mongella. SOMA: Mwinyi: SMZ mstari wa mbele fursa kiuchumi kwa wanawake

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *