Rais Mwinyi ataja vipaumbele 6 vya usimamizi

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametaja vipaumbele sita, vikiwa ni mwongozo wa utekelezaji na usimamizi wa majukumu kwa viongozi wakuu wa serikali katika taasisi wanazoziongoza. Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Raqey Mohamed ameeleza Dk Mwinyi alitaja vipaumbele hivyo alipofungua mafunzo ya awali kwa viongozi wakuu wa serikali katika Chuo cha IIT Madras, Bweleo, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Alivitaja vipaumbele hivyo ni kasi ya utekelezaji, uwajibikaji, ufanisi katika utendaji, usimamizi bora wa watumishi, matumizi sahihi ya takwimu katika maamuzi na kuimarisha matumizi ya teknolojia na mifumo ya kidijiti. “Mafunzo haya yana lengo la kuimarisha usimamizi bora wa utendaji, kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, hivyo yanapaswa kupewa umuhimu mkubwa,” alisema Dk Mwinyi.

Amesema kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Nane inahitaji kasi ya utekelezaji, uwajibikaji na usimamizi bora wa majukumu ili kupata matokeo chanya katika kuwahudumia wananchi. Amewasisitiza watendaji hao kuwa na uelewa wa juu wa mbinu za kisasa za kuongeza ufanisi na kasi ya utendaji pamoja na uwezo wa kufanya uamuzi sahihi. “Wakati umefika wa kufanya mageuzi makubwa katika matumizi ya takwimu katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo kwa ufanisi katika sekta zote za umma,” alisema.

Amesisitiza umuhimu wa kuongeza ufanisi katika taasisi wanazoongoza, kuimarisha usimamizi wa watumishi na kuendeleza nidhamu katika sekta ya umma. Aidha, Dk Mwinyi amehimiza kukuza uelewa juu ya matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza ufanisi na kupunguza muda wa utekelezaji wa majukumu.

Akizungumzia miradi ya maendeleo, Dk Mwinyi ameagiza watendaji wakuu kuwa na ratiba ya ufuatiliaji wa miradi kwa ajili ya utatuzi wa changamoto, akisisitiza kutokuwa na miradi inayosimama bila kupatiwa ufumbuzi. SOMA: Wadau kuungana kukomesha udhalilishaji Zanzibar.

Amewasisitiza viongozi hao kuwa karibu na vyombo vya habari kwa lengo la kufikisha taarifa sahihi kwa umma, kudumisha ushirikiano na wadau wa maendeleo na kutumia mbinu za kujenga uhusiano mzuri wa kimkakati na washirika wa maendeleo ili kuitangaza Zanzibar kimataifa.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. ✈️Sensa ya UMILIKI MALI KUWA MICHOCHEO CHA UCHUMI? UmECHOKA KUDHANI WATU NI MASIKINI NA HAWAMILIKI CHOCHOTE SENSA HII NI JAWABU!✈️ Sensa ya UMILIKI MALI KUWA MICHOCHEO CHA UCHUMI? UmECHOKA KUDHANI WATU NI MASIKINI NA HAWAMILIKI CHOCHOTE SENSA HII NI JAWABU✈️BY Mwigulu🛬✈️Sensa ya UMILIKI MALI KUWA MICHOCHEO CHA UCHUMI? UmECHOKA KUDHANI WATU NI MASIKINI NA HAWAMILIKI CHOCHOTE SENSA HII NI JAWABU!✈️ Sensa ya UMILIKI MALI KUWA MICHOCHEO CHA UCHUMI? UmECHOKA KUDHANI WATU NI MASIKINI NA HAWAMILIKI CHOCHOTE SENSA HII NI JAWABU✈️BY Mwigulu🛬✈️Sensa ya UMILIKI MALI KUWA MICHOCHEO CHA UCHUMI? UmECHOKA KUDHANI WATU NI MASIKINI NA HAWAMILIKI CHOCHOTE SENSA HII NI JAWABU!✈️ Sensa ya UMILIKI MALI KUWA MICHOCHEO CHA UCHUMI? UmECHOKA KUDHANI WATU NI MASIKINI NA HAWAMILIKI CHOCHOTE SENSA HII NI JAWABU✈️BY Mwigulu🛬✈️Sensa ya UMILIKI MALI KUWA MICHOCHEO CHA UCHUMI? UmECHOKA KUDHANI WATU NI MASIKINI NA HAWAMILIKI CHOCHOTE SENSA HII NI JAWABU!✈️ Sensa ya UMILIKI MALI KUWA MICHOCHEO CHA UCHUMI? UmECHOKA KUDHANI WATU NI MASIKINI NA HAWAMILIKI CHOCHOTE SENSA HII NI JAWABU✈️BY Mwigulu🛬

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button