Nabi awapongeza wachezaji

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana kuipigania timu yao kupata ushindi kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga juzi iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 32, huku wakiweka rekodi ya kucheza mechi 49 za ligi bila ya kufungwa.

Akizungumza baada ya mchezo huo kocha huyo alisema kuwa pamoja na ratiba ngumu inayowakabili, wachezaji wake wameonesha mapenzi makubwa na timu yao kutokana na kucheza kwa kujituma na kupambania ushindi na mafanikio ya Yanga.

“Wanastaili pongezi kwa namna wanavyojituma kupigania ushindi kushinda mechi au kutopoteza mechi hakuja wavimbisha vichwa ndio kwanza wamekuwa makini kusikiliza maelekezo tunayo wapa na wanapokwa uwanjani wanayafanyia kazi na tunapata ushindi hongera sana kwao,” alisema Nabi.

Kocha huyo ameeleza siri ya ushindi dhidi ya Mbeya City imetokana na kuwaona wapinzani wao hao namna wanavyocheza katika mechi kadhaa, ikiwemo dhidi ya Simba na kupanga mpango maalumu, ambao anashukuru umefanikiwa.

Alisema ingawa haikuwa rahisi lakini uzoefu na wachezaji wake pamoja na kufuata maelekezo anayowapa mazoezini vimechangia wao kupata ushindi huo muhimu.

Kwa upande wake Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amewapongeza Yanga kwa ushindi huo huku akisema sababu ya kipigo hicho ni ubora waliokuwa nao wachezaji wa wapinzani wao.

Alisema lengo lao ilikuwa ni ushindi lakini imeshindikana wanakubali matokeo na wanajipanga kwa mechi nyingine zinazo fuata kwenye ligi hiyo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x