Naibu mufti Zanzibar ataka malezi bora jamii yenye maadili

ZANZIBAR: Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amesema ili kupata maelezi bora ya jamii inatokana na malezi bora ya pamoja kwa watoto na vijana katika kujenga misingi kwenye dini tangu wakiwa wenye umri mdogo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mashindano ya Kuhifadhi Qur An yaliyofanyika Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar, Machi 18, 2026 ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria.

Amesema ukiangalia katika jamii bado kuna mporomoko wa maadili mkubwa lakini watu wanapokutana pamoja na kuelezana basi itasaidia kujenga msingi mzuri na kuwa na jamii yenye maadili mema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Hamasi Yussuf Masauni amesema mashindano hayo yamekuwa ni mwendelezo wa miaka mingi ambapo imesaidia vijana wengi kuku ana kuwajenga kimaadili.

Masauni amesema pamoja na mambo mengine Jimbo la Kikwajuni limekuwa likisaidia Watoto wenye uhitaji mbalimbali ikiwemo katika kupata elimu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button