Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amezindua Boti ya Doria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania , Jijini Mwanza, itakayofanyakqzi ya kusaidia kudhibiti biashara ya magendo katika Mwambao wa Ziwa Victoria.
Ametoa wito kwa Watanzania, kupiga vita na kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa kuwa vinalisababishia Taifa hasara kutokana na kupoteza fedha ambazo zingetumika kuihudumia Jamii.(Picha na Wizara ya Fedha)