Nandy: Mashabiki msiulizie masuala ya familia yangu

Nandy: Mashabiki msiulizie masuala ya familia yangu

MWIMBAJI wa muziki nchini, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ambaye ni mama wa mtoto mmoja amewaomba mashabiki wake waache kuulizia masuala ya familia yake, hasa mtoto wake.

Nandy ambaye ni mke wa msanii Billnas ameeleza: “Mashabiki wasichanganye maisha ya Insta na maisha ya ndoa yangu. Huku Insta maisha yangu hata robo hayajafika.

“Msipagawe na hizi content ninazopost au ninavyosafiri. Popote nilipo yupo ananyonya mpaka anakataa ziwa mwenyewe, anashinda na mimi mpaka nikitokea akisikia sauti anaruka kama kichaa then bond is real, endeleeni kusapoti muziki mambo ya familia yangu achene,”ameandika Nandy.

Advertisement