DAR ES SALAAM: NUSU fainali ya mashindano ya Kombe la Dar Port Kagame la Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inapigwa leo Dar es Salaam.
Katika nusu fainali ya kwanza APR ya Rwanda itaikabili Al Hilal ya Sudan kwenye uwanja wa KMC Complex, Kinondoni wakati Al- Wadi ya Sudan itaivaa Red Arrows ya Zambia kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Washindi wa mechi hizo watacheza fainali ya kombe hilo Julai 21 Dar es Salaam.
SOMA: Karia: Tutapandisha hadhi michuano ya CECAFA
Kuelekea nusu fainali ya kwanza kati ya APR ya Rwanda na Al Hilal (Sudan) kwenye Uwanja wa KMC, mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya kusisimua kwani timu hizi mbili hazikupata kipigo katika mechi zao tatu za makundi.
Al Hilal ambayo haijawahi kutwaa kombe la CECAFA ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ASAS Djibouti Telecom katika mechi ya ufunguzi, ikaikanda Red Arrows (Zambia) 5-0 na kumaliza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Kwa APR ambayo imeshinda kombe hilo mara tatu, ilianza kwa kuizima Singida Black Stars bao 1-0, ikaifunga El Merriekh Bentiu (Sudan Kusini) 1-0 na kumaliza hatua ya makundi kwa sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda, SC Villa.
Florent Ibenge, the Al Hilal coach has made it clear that they are determined to jump past the semi-final and get to the final. “We are hungry to go all the way and try to win the Cup. The team is very motivated and we are ready,” said Ibenge.
Kocha wa Al Hilal Florent Ibenge ameweka wazi kuwa klabu yake imeazimia kuvuka kikwazo cha nusu fainali na kutinga fainali.
“Tuna nja ya kushinda na kubeba taji. Timu imehamasika sana na tuko tayar,” amesema Ibenge.
Kocha wa APR, Darko Novic ambaye alijiunga na Klabu hiyo mwezi uliopita tu ameweka wazi kuwa kucheza dhidi ya Al Hilal itakuwa kibarua kigumu.
“Wanafurahia mwendo mzuri na wameshinda mechi zao zote tatu kwenye makundi. Lakini tutajipanga ipasavyo kwa sababu tumetazama baadhi ya mechi zao na kujua nini cha kutarajia,” aliongeza Novic.
Katika nusu fainali ya pili, licha ya kutinga hatua ya mtoano kwa kuwa timu iliyoshika nafasi ya pili, kocha wa Red Arrows Chisi Mbewe amesema watakuwa tofauti sana katika hatua ya mtoano.
“Tulianza polepole sana kwa sababu wachezaji walirudi haraka kutoka likizo kujiandaa na mashindano haya. Lakini tumeimarika vyema na tunapaswa kuonyesha utofauti,” ameongeza kocha huyo.
Red Arrows iliifunga Gor Mahia bao 1-0 katika mechi ya kwanza kisha kuchapwa bao 5-0 na Al Hilal. Hata hivyo klabu hiyo ya Zambia ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya ASAS Djibouti Telecom katika mechi ya mwisho ya makundi ili kujihakikishia nafasi katika nusu fainali.