NBC yaahidi ushirikiano utekelezaji miradi ya kimkakati

Katika kufanikisha miradi mbalimbali ya kimkakati Benki ya Taifa  Biashara  ya Taifa  (NBC) imeahidi kuwa mstari wa mbele kwa kutoa ushirikiano serikalini na wakandarasi kwa lengo la kuhakikisha miradi ya kimkakati inayotekelezwa kwa manufaa ya Watanzania inakamilika kwa wakati.

Benki ya NBC ni miongoni mwa taasisi zilizoshiriki hafla ya uwekaji jiwe la msingi kuashiria kuanza kutekelezwa kwa kwa mradi wa ujenzi wa wa reli ya kisasa (SGR) kwa kipande cha nne kinachoanzia Taborahadi Isaka katika wilaya ya Kahama, Shinyanga.

Akihutubia wananchi katika tukio hilo, Makamu wa Rais Dk Philip Mpango aliitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi wa TRC kuendelea kutimiza wajibu wao wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Aidha ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohujumu mradi wa SGR.

“Naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kubaini mtandao wa wizi kwenye mradi wa SGR na kuwakamata wote pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria,” amesema Dk Mpango.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji  wa  NBC  Simon Ntwale alimweleza  Makamu wa Rais Dk Mpango namna benki hiyo inavyoshiriki kikamilifu katika ujenzi huo wa mradi mkubwa.

“Sisi benki ya NBC tumeshiriki kikamilifu katika kumwezesha mkandarasi Yapi Merkezi kununua mitambo ya kufanyia ujenzi huo. Pia tumewezesha zoezi la ulipaji fidia kwa wanaopitiwa na mradi huu,” Ntwale amemweleza Dr Mpango baada ya kutembelea banda la NBC.

Aliongeza kuwa kuwa NBC imewezesha ununuzi wa vichwa na mabehewa ya kisasa kwa ajili ya mradi huo.

Awali akitoa taarifa za Ujenzi wa Mradi huo,  Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa amesema uwezo wa kubeba mizigo kupitia reli ya kisasa utakua hadi kufikia tani 120 kwa behewa ikiwa ni mara tatu ya reli ya sasa yenye uwezo wa kubeba tani 40 tu kwa behewa moja.

Alisema kuwa kupitia ujenzi huo,TRC inatarajia kuboresha chuo cha reli kilichopo Tabora na kuweza kutoa shahada ya uandisi katika reli mara baada ya kukamilika.

Vilevile amesema TRC imeendelea kuokoa gharama kwa kiasi kikubwa kupitia mikataba ya ujenzi wa reli ambayo hairuhusu ongezeko la gharama kutoka kwa mkandarasi kutokana na mabadiliko ya bei za vifaa na malighafi.

Habari Zifananazo

Back to top button