Nchi 10 za Afrika zawezeshwa udhibiti vifaa tiba na Tanzania

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini (TMDA) imewapa mafunzo nchi 10 za Afrika ya kufanya tathmini ya udhibiti wa vifaa tiba kwa akina mama, watoto wachanga na watoto kwa wataalam wa vifaa tiba kutoka mamlaka za udhibiti za nchi 10 za Afrika.

Wataalam hao wanatoka katika mamlaka za udhibiti wa vifaa tiba na vitendanishi kwa nchi za Afrika Uganda, Kenya, Ethiopia, Nigeria, Afrika Kusini, Botswana, Zambia, Rwanda, Ghana, Senegali na Tanzania.

Kongamano hilo ni la kwanza Barani Afrika ambapo mafunzo hayo yanafanyika kufuatia nchi za Afrika kutokuwa na uwezo wa kudhibiti bidhaa za wakinamama na watoto hivyo mafunzo hayo yatasaidia uwezo wa kutathimini bidhaa kabla hazijaingia kwenye soko.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Mkurugenzi wa Vifaa tiba na vitendanishi Kissa Mwamwitwa amesema watabadilishana uzoefu ilikupata watalaam watakaokuwa wana uwezo wa kusaidia eneo hilo la vifaa tiba kwa akinamama na watoto kabla havijaingia sokoni.

Aidha ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Afya kwa kuipa uwezo TMDA kujulikana Afrika na kuweza kutoa utaalamu ambao wanatoa kwa Nchi zingine.

“Warsha hii imedhaminiwa na Wadau wa maendeleo USAID-MTaPS, kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), Jukwaa la Afrika la Udhibiti wa Vifaa tiba, AUDA-NEPAD na TMDA.

Tunaishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Rais wetu Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Afya kwa kutupatia uwezo ambao tunaonekana Bara la Afrika.’’ amesema Kissa Mwamwitwa.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button