Ndege yapotea ikiwa na Makamu wa Rais Malawi

LILONGWE, Malawi – Ndege ya kijeshi iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi na watu wengine tisa imepotea, na jitihada za utafutaji zinaendelea, ofisi ya rais imesema. 

Ndege hiyo iliyombeba Makamu wa Rais Saulos Chilima mwenye umri wa miaka 51 iliondoka mji mkuu, Lilongwe, siku ya Jumatatu lakini ilishindwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mzuzu takriban kilomita 370 (maili 230) kuelekea kaskazini baada ya dakika 45.

Ndege hiyo iliondoka saa 3:00 asubuhi kwa saa za Malawi (07:00 GMT). Mamlaka za anga zilipoteza mawasiliano na ndege hiyo ilipokuwa “imeondoka kwenye rada,” taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ilisema.

SOMA: LATRA yatangaza bei Daraja la Kawaida SGR

Chakwera aliarifiwa kuhusu kupotea kwa ndege hiyo na mkuu wa majeshi ya Malawi, kisha akaamuru operesheni ya utafutaji na akaahirisha safari yake kwenda Bahamas.

“Tumeshindwa kupata mawasiliano na ndege hiyo tangu ilipopotea kwenye rada,” taarifa ilisema.

Rais aliagiza mamlaka za kitaifa na za mikoa “kufanya utafutaji wa haraka na operesheni ya uokoaji ili kubaini mahali ilipo ndege hiyo,” ofisi yake ilisema.

Habari Zifananazo

Back to top button