NDEGE ya kwanza ikiwa na vifaa vya matibabu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) imewasili Beirut saa moja iliyopita kutibu maelfu ya watu waliojeruhiwa katika mashambulizi ya Israel Lebanon.
Taarifa ya Mkurugenzi wa WHO, Tedros Ghebreyesus imeeleza ndege zingine mbili zimepangwa kuwasili leo mchana zikiwa na vifaa vya matibabu, afya ya akili na kipindupindu. Ndege nyingine pia inatarajiwa kutua Beirut kesho.
“Tunashukuru UAE na Dubai Hub kwa usaidizi wao wa haraka wa kutosha kufanikisha hili,” ameandika Tedros kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X.
Wizara ya Afya nchini Lebanon ilisema hadi kufikia jana watu tisa walipoteza maisha na 14 kujeruhiwa katika mashambulizi hayo.
View this post on Instagram