Serikali yaanika siri ya mafanikio

SERIKALI imesema imeruhusu sekta ya umma na binafsi kushirikiana katika kujenga nyumba ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu na kukabiliana na uhaba wa nyumba nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Lucy Kabyemera kwenye mkutano wa 42 wa Shelter
Afrique unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton Jijini Abuja, Nigeria.

Kabyemera anaiwakilisha nchi katika Mkutano huo akiambatana na watendaji
wa Wizara hiyo na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
.
Amesema kuwa serikali inatambua kwa dhati umuhimu na mchango wa sekta
binafsi kwenye maendeleo ya ujenzi wa makazi na ukuzaji wa uchumi na
maendeleo ya watu.

Amesema, ili kuweza kuharakisha maendeleo ya sekta ya nyumba sekta ya benki imewekewa mazingira rafiki ya kisheria ili kushiriki kikamilifu kutoa mikopo ya ujenzi na ununuzi wa nyumba.

Katika kutekeleza ushirikiano wa pande hizo mbili sera iliyoboreshwa ya ubia
ya Shirika la Nyumba la Taifa ilizinduliwa Jumatano ya Novemba 16, 2022, jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Wakati huo huo Serikali za Bara la Afrika zimeshauriwa kuipa kipaumbele
sekta ya nyumba ili kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza miaka
michache ijayo ya ongezeko kubwa la watu hasa mijini.

Hayo yamesemwa na wajumbe na viongozi mbalimbali wanaosimamia sekta ya nyumba na makazi wanaohudhuria Mkutano wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique) unaofanyika Jijini Abuja.

Changamoto za upatikanaji wa taarifa za nyumba bora na makazi, kutokuwepo mikopo nafuu ya nyumba za gharama nafuu na ushiriki mdogo wa sekta binafsi katika ujenzi wa nyumba za watu wa kipato cha chini imeelezwa kuchangia zaidi ya asilimia 50 ya miji mingi Barani Afrika kuwa na makazi holela.

Ili kukabiliana na hali hiyo Mkutano huo Mkuu wa Mwaka Wa 42 wa Shirika
hilo umezishauri nchi za Bara la Afrika kushawishi na kuweka mazingira rafiki
ya sekta binafsi ili ishiriki kupunguza changamoto za upatikanaji wa nyumba
za gharama nafuu.

Aidha, serikali za Bara la Afrika zimeshauriwa kuboresha huduma za kijamii ikiwemo nyumba bora katika maeneo ya vijijini ili kupunguza wimbi la watu wanaohamia mijini kutafuta maisha bora.

Kutokana na umuhimu wa sekta ya nyumba jatika kuchangia ukiaji wa
uchumi, upatikanaji wa ajira na kudumisha amani na utulivu katika miji, serikali za Afrika zimeshauriwa kuiona sekta ya nyumba kama jambo
mtambuka linalohitaji kupewa kipaumbele katika mipango ya nchi hizo

Wamesisitiza kuwa malengo ya milenia hayawezi kufikiwa kama sekta ya
nyumba haitapewa kipaumbele.

Wakasisitiza kuwa mashirika ya nyumba
Barani Afrika yameshindwa kuwapatia wananchi wake nyumba bora za
gharama nafuu kutokana na mashirika hayo kubebeshwa mzigo wa kutafuta
ardhi nafuu, kuweka miundombinu ya maji, barabara na umeme katika
maeneo ya ujenzi wa nyumba hali inayofanya nyumba hizo kuwa na gharama
kubwa.

Hivyo nchi hizo zimeshauri kuwa serikali za mataifa ya Afrika ziondoe vikwazo
mbalimbali vinavyokabili mashirika hayo ya nyumba ili kuyasaidia kukwamua
Bara hilo katika kuondoa uhaba wa nyumba za gharama nafuu.

Mojawapo ya hatua za kukwamua mashirika hayo ni kushirikisha sekta binafsi ili kuchangia mfuko wa maendeleo ya nyumba wa kila nchi, kuwa na sera endelevu za ukuaji wa sekta ya nyumba na kuwa na uratibu mzuri wa mikopo nafuu ya nyumba. .

Kadhalika, nchi za Afrika zimetakiwa kushirikiana katika kubadilishana
uzoefu na kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa changamoto za sekta ya nyumba ili
kuzitatua.

Kadhalika, nchi za Afrika zimetakiwa kushirikiana katika kubadilishana
uzoefu na kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa changamoto za sekta ya nyumba ili kutatua.

 

Habari Zifananazo

Back to top button