NIC waja na Bima ya Maisha

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limetambulisha aina mpya ya bima ijulikanayo kama ” Bima ya Maisha” inayotoa dhamana ya kifedha kwa wahusika au wategemezi wa mteja endapo mteja huyo atakuwa amekumbwa na janga la kifo.

Akitambulisha bima hiyo kwa wakurugenzi wa taasisi na wakuu wa taasisi na kampuni mbalimbali jijini Arusha ,Mkurugenzi wa NIC , Kaimu Mkeyenge alisema bidhaa ya Bima ya Maisha ni bidhaa inayopatikana sokoni na itawasaidia pale wanapopata majanga.

Advertisement

Amesema NIC wameamua kuelezea umuhimu wa bima hiyo ili kuwasaidia wakuu wa taasisi kutoa michango yao NIC kadri watakavyotaka kuchangia kwa vipengele vitatu kisha pale watakapopata janga la kifo wataweza kupewa fedha zao kupitia wao au hata wategemezi wao.

SOMA: NIC: Bima humrudisha mbima alipokuwepo awali

Amesema bidhaa hiyo inaweza kuwashika mkono pale wanapokumbwa na majanga na wananchi pia wanajiunga na bidhaa hiyo na kupata mkono wa pole pale wanapopata janga hilo la kifo.

SOMA:Mpango mzima, NIC Kiganjani

“Tumekuwa tukipata misiba ya kuondokewawna wenza , watoto au wazazi hivyo tumekuwa tukichangishana wenyewe kwa wenyewe nikaona hii bima ya Maisha itasaidia kuchangia pale majanga yatakapotea ili kunusuru kila mmoja kuingia mfukoni kuchangia badala yake bima hii ifanye kazi hiyo,”