NLD yaahidi makubwa barabara kuunganisha mikoa

DODOMA: CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kimesema serikali yake itajenga njia mbili Barabara ya Dodoma–Mwanza ili kukuza muunganiko wa mikoa ya Kati na Magharibi.
Ilani ya uchaguzi ya chama hicho imeeleza Barabara ya Segera–Arusha itajengwa kuwa ya njia mbili kupunguza ajali, kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa na kuunganisha Kanda ya Kaskazini kwa usalama na ufanisi.
NLD imeahidi kuipandisha hadhi Barabara ya Segera– Chalinze kuwa na njia mbili kwa sababu ni kiungo kati ya Kanda ya Kaskazini na Kati na ni njia kuu ya kimataifa kwa mizigo kutoka Bandari ya Tanga. SOMA: NLD yaahidi elimu bure hadi vyuo vya kati
Chama hicho kimesema Barabara ya Chalinze–Morogoro–Tunduma (Mpaka wa Zambia) itakuwa na njia mbili hadi njiapanda ya Tunduma. Kimesema kutoka hapo itaendelea kuwa barabara ya njia mbili hadi kwenye mpaka ili kuhudumia mizigo ya kimataifa, kupunguza msongamano na kuimarisha uchumi wa mikoa ya Kati na Kusini.
Ilani ya NLD imeeleza chama hicho kitaboresha barabara vijijini kwa kujenga barabara za lami na zege zinazopitika mwaka mzima kwa kila tarafa na kata. Chama hicho kimeahidi kuanzisha Mfuko wa Barabara za Vijijini kwa kushirikianana halmashauri, wadau wa maendeleo na sekta binafsi.
NLD imeahidi Barabara ya Dar es Salaam–Chalinze itajengwa kuwa ya njia nne ili kuondoa msongamano wa magari Dar es Salaam na kuwezesha usafiri wa haraka wa watu na mizigo kuelekea mikoa ya Kati, Kaskazini na Kusini.
Chama hicho kimeahidi kujenga lami kwenye barabara zote za wilaya na za kuunganisha madaraja ya vijijini na mijini kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayodumu na kuimari sha bandari za Ziwa Tangan yika, Ziwa Victoria, Mtwara na Tanga kwa kushirikiana na sekta binafsi.



