KATIKA kudhibiti matumizi sahihi ya fedha za umma Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ina watalamu wabobezi 400 wenye CPA ikiwemo wengine wenye taaluma mbalimbali nchini.
Akizungumza kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Arusha juu ya kuandika zaidi taarifa za CAG Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kitengo cha Huduma za Kiufundi (TSSU), Deogratisu Kirama amesititiza ofisi hiyo imeajiri wataalamu hao na wengine ili kuleta tija zaidi katika ukaguzi na udhibiti wa fedha za umma.
Amesema ni vema wanahabari wanachambua na kuandika zaidi taarifa za CAG ili kujua matumizi ya fedha za umma au za miradi zimefanya kazi yake ikiwemo miradi isiyotekelezwa katika kuchochea maendeleo na kusisitiza ripoti ya CAG ni muhimu kuchambuliwa na hata kama kunahati safi lakini ukienda chini kunakasoro za sheria ya bajeti na manunuzi.
“CAG ameajiri wataalam wengi ikiwemo wenye CPA ili kuleta tija zaidi katika kaguzi lakini pia tunafanya ukaguzi wa kifanisi ambao ni uwekevu,tija na ufanisi katika maeneo yaliyochaguliwa na sio kwa kila taasisi ”
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria,Elieshi Saidimu amewataka wanahabari kuandika zaidi taarifa zinazotolewa na CAG ikiwemo kujua sheria,kanuni na taratibu zinazoratibu uendeshaji wa ofisi hiyo sanjari na kuchambua taarifa zinazotolewa na CAG.