Okocha ateuliwa waziri wa michezo
MCHEZAJI wa zamani wa Nigeria na klabu kadhaa barani Ulaya, Augustine Okocha ‘Jay Jay’ ,46, ameteuliwa kuwa Waziri wa Michezo, Vijana na Maendeleo nchini humo.
Uteuzi huo umefanywa na Rais mpya wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria, Bola Tinubu.
Okocha aliwahi kucheza katika klabu za Eintracht Frankfurt, Fenerbahçe, Paris Saint Germain (PSG) na Bolton.
Jay Jay ambaye ana mabao 14 katika michezo 73 aliyocheza kati ya 1993 na 2006 akiwa timu ya taifa ya Nigeria ni bingwa wa Olimpiki mwaka wa 1996, mshindi wa CAN 1994, 2000.