P.Diddy kutoboa kugumu

MAREKANI : MWANAMUZIKI wa nyimbo za Rap nchini Marekani, Sean Diddy Combs amenyimwa dhamana kwa mara ya tatu kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu akiwa gerezani.

Hapo awali timu ya majaji wawili walikataa nguli huyo wa muziki kuachiliwa kwa dhamana kwa sababu ya kuwepo kwa wasiwasi wa kuwachezea mashahidi, wakiona kuwa ni hatari kubwa ikiwa ataachiliwa kabla ya kesi, ambayo imepangwa kufanyika Mei 2025.

Mpaka sasa,Sean Diddy Combs anazuiliwa katika Kituo cha Metropolitan huko Brooklyn, New York akishtakiwa kwa makosa matatu ikiwa ni pamoja na kula njama, biashara ya ngono na usafirishaji kwa shughli za ukahaba.

Advertisement

Hatahivyo, mwanamuziki huyo ameendelea kukana makosa yake na kudai kuwa makosa  yote aliyofunguliwa hayana ukweli wowote.

Mmoja wa hakimu  aliwasilisha ushahidi wa kesi hiyo na kudai kuwa Sean Diddy Combs aliamua kuingilia ushahidi akiwa gerezani jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria.

Jaji wa Wilaya ya Marekani Arun Subramanian alihitimisha mahakama haiwezi kumwamini Combs ikiwa angeachiliwa kwa dhamana.

“Mahakama inaona kwamba serikali imejiridhisha kuwa ushahidi uliowasilishwa unaonyesha  wazi kuwa huwezi kuaminika kuachiliwa kwa  dhamana”, alisema Jaji Arun.

Nao waendesha mashtaka wamepinga kumpa Combs kupatiwa dhamana kutokana na utovu wa nidhamu akiwa gerezani. SOMA : P Didy avunja sheria za gereza

Katika kesi iliyowasilishwa mahakamani , waendesha mashtaka walimshutumu mwanamuziki huyo wa rap kwa kutumia vibaya mawasiliano ya jela kushawishi mashahidi katika kesi yake.

Hatahivyo, mawakili wa utetezi wa Combs wamesema anapaswa kuachiliwa kwa dhamana kwa mujibu wa sheria ili aweze kujiandaa vyema na kesi yake mwakani.