PICHA: Amiri Jeshi Samia kwenye kilele miaka 60 JWTZ
AMIRI Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono viongozi mbalimbali walioshiriki kilele cha miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Gwalide la Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) likitoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Kilele cha Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.