PICHA: Bodaboda anaswa, afungishwa vioo

 

 

MKAGUZI wa vyombo vya moto Mkoa wa Mtwara, Steven Changanga amemfungisha kwa lazima vioo vya pembeni dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda aitwaye Ramadhani Mussa aliyekamatwa na polisi wa usalama barabarani mkoani humo kwa kosa la kung’oa kwa makusudi vioo hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mratibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Emilian Kamuhanda amesema wamebaini madereva wengi wa pikipiki huvitoa kwa makusudi vioo vya pembeni kwenye vyombo vyao kwa kisingizio kuwa nyumba wanazoishi zinamilango midogo hivyo upelekea kupata changamoto wakati wa kuzihifadhi.

Hata hivyo amesema hoja hizo hazina mashiko na kuwakamata wote wasionazo na kuwatoza faini kwa mujibu wa sheria.

Habari Zifananazo

Back to top button