PICHA| Waziri Mkuu akagua barabara ya Somanga-Dar

LINDI — Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili leo asubuhi Aprili 16, 2025, katika eneo la Somanga kwa ajili ya kukagua hali ya miundombinu ya barabara kuu ya Dar es Salaam-Lindi, ambayo imeathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stegomena Tax, pamoja na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, kwa ajili ya kutathmini athari za mvua hiyo na hatua zinazochukuliwa ili kurekebisha miundombinu ya barabara hiyo muhimu kwa usafirishaji wa bidhaa na abiria kati ya mikoa ya Dar es Salaam na Lindi.
Aidha, Majaliwa amesema serikali itaendelea kufanya juhudi za haraka kutatua changamoto za miundombinu ili kuhakikisha usalama na urahisi wa usafiri kwa wananchi.