Polisi yazungumzia taarifa tishio la ugaidi

JESHI la Polisi nchini limeondoa hofu juu ya uvumi wa mashambulizi ya kigaidi nchini kufuatia taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani ikiwahadharisha raia wake juu ya hatari hiyo.

Akizungumza leo Januari 26, 2023, Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime amewahakikishia wananchi usalama wao na kuwataka watulie na waendelee na shughuli zao za kila siku.

Aliwataka wananchi kuendelea kuwa waangalifu na kutoa taarifa kwa mamlaka husika, ili kuchukua hatua stahiki za usalama endapo watahisi hali yoyote isiyo ya kawaida.

Jana Jumatano Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulitoa taarifa ikiwaonya raia wake, kwamba makundi ya kigaidi yanaweza kushambulia kwa tahadhari kidogo au bila kutoa tahadahri kwa kulenga maeneo ya hoteli, balozi, migahawa, maduka makubwa na soko, vituo vya polisi, maeneo ya ibada na maeneo mengine ambayo wanayatembelea.

Katika ripoti yake, Ubalozi huo uliwataka raia wa Marekani nchini Tanzania kuwa makini na mazingira yao, kuchukua hatua za usalama wa kibinafsi huku wakiweka hadhi ya

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jumanne
Jumanne
7 months ago

How did you know these information? My advice before telling the majority took to government how to solve this issues. This is our country pls respect our country

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x