WIZARA ya Fedha kupitia Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi(PPP) imefanya kikao kazi cha kupitia Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi, pamoja na kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Miaka Mitano wa Sera ya Taifa ya PPP.
Kaimu Kamishna wa Kitengo cha PPP, Bashiru Taratibu akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Taratibu amesema kuwa lengo la kikao kazi hicho lilikuwa kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Sera ya Taifa ya PPP na maboresho ya Sheria ya PPP, Sura 103 iliyopitishwa na Bunge pamoja na kuona changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wake ili wakati wa kufanya maboresho waweze kubaini maeneo yenye changamoto katika utekelezaji ili yaweze kupatiwa ufumbuzi katika utekelezaji ujao.
“Kikao kazi hiki kinahusu masuala yote ya Kisera, Sheria na Kanuni leo tumewaita wenzetu wa Wizara mbalimbali na Taasisi zilizo chini yao kwa ajili ya kuja kupitia Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya PPP ulioandaliwa mwaka 2021.

Mkakati wa Miaka Mitano wa mwaka 2021/22- 2025/26 kwa hiyo sasa hivi tunakaribia mwisho wa Mkakati huo lakini katika ujio wetu wa leo na katika siku hizi tano tutakazofanya kikao kazi hiki katika ngazi ya Wizara tutapitia Mkakati huo kuona utekelezaji wake, kukumbushana majukumu ya kila mdau kwenye ule Mkakati,” amesema Taratibu.
Amesema kuwa vile vile mwaka 2023 walifanya marekebisho ya Sheria, na kwamba yale marekebisho pia wamekuja kukumbushana na kujulishana kuwa marekebisho hayo ni yapi, ili Wizara ambazo ndio zenye majukumu mbalimbali ambayo yanatekelezwa na Taasisi zao ziyaelewe na kutumia vizuri fursa zinazopatikana kupitia dhana ya PPP.
Aidha, amesema kuwa pamoja na kupitia marekebisho ya Mkakati, pia amewafahamisha moja ya jukumu la PPP kuwa ni kuishirikisha Sekta Binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo huko nyuma yalikuwa ni majukumu ya Serikali.

“Tunaamini wenzetu hawa ambao wengi wametoka katika Wizara mbalimbali wakiielewa hii dhana vizuri ina maana kuwa yale majukumu ambayo yana uwezo wa kutekelezwa kwa kutumia Sekta Binafsi watahakikisha kuwa yanakwenda kutekelezwa kwa kuishirikisha Sekta binafsi, jambo ambalo ndiyo madhumuni makubwa ya Sera” amesisitiza Taratibu.
Kikao kazi hicho kimeshirikisha baadhi ya Wizara ambazo zina miradi ya maendeleo hasa miradi ya masuala ya miundombinu kama vile Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Afya.
If you are going for finest contents like me, just pay a visit this
web page every day for the reason that it provides feature contents, thanks
Hi, I think your site might be having browser compatibility issues.
When I look at your blog in Chrome, it looks fine but when opening in Internet Explorer,
it has some overlapping. I just wanted to give you
a quick heads up! Other then that, awesome blog!