Prof. Assad: Wajumbe wa Bodi wafanyiwe Mchujo

ARUSHA: Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Profesa Mussa Assad amesema ni wakati sasa wajumbe wa Bodi katika taasisi za Umma wakapatikana kwa utaratibu wa usaili ili kupata viongozi watakao ongeza tija kwa taasisi.
–
Akizungumza wakati wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC), Prof. Assad amesema upatikanaji wa wajumbe wa bodi ni muhimu ili kuwa na usimamizi thabiti wa mashirika hayo.
–
“Ukifanya usaili utachuja. Wajumbe wa bodi wanapaswa kufanyiwa usaili,” amesema “Usipofanya hivyo unajikuta una wenyeviti wa bodi wa tangu miaka ya 60.” Mkaguzi huyo Mkuu wa zamani wa Hesabu za Serikali amesema bodi ni muhimu kuwezesha usimamizi mzuri wa rasilimali za taasisi.