Prof. Mhando ang’atuka, kumpisha Shivji ZIFF

DAR ES SALAAM: Profesa Mhando atangaza kung’atuka nafasi ya Mkurugenzi wa Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) na nafasi kukaimiwa na Muongozaji na Mtayarishaji wa filamu, Amil Shivji.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa habari leo Oktoba 03, 2023 jijini Dar es Salaam, Prof. Mhando amesema anang’atuka nafasi hiyo sio kwakuwa amechoka ila ni katika kutoa fursa kwa vijana kwakuwa wao wana kasi na maono zaidi katika kuchapa kazi.

“Vijana wanayo nafasi kubwa zaidi ya kuongoza kwa sababu wao wana nafasi kubwa zaidi,” amenukuliwa, Prof. Mhando.

“Napokea kijiti hiki na nataka kuhakikisha uchapaji kazi ili kutangaza uwezo wetu na vipawa vyetu ulimwenguni,” amesema, Shivji.

Aidha, Shivji amesema anaenda kuleta mabadiliko katika muundo wa uongozi, kusaidia wasanii na uandaaji wa matamasha katika kuchagua aina za  filamu, pia mtindo bora wa utumbuizaji wa muziki.

Mbali na Utayarishaji na Uongozaji wa filamu, Shivji pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Anavutiwa haswa kutumia kazi yake kupinga uwasilishaji potofu wa historia ya Bara laAfrika. Filamu zake fupi za “Shoeshine” na “Samaki Mchangani” zimetambulika duniani kote na kujizolea sifa nyingi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button