Prof Mkenda awasilisha bajeti ya tril 1.7/-
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya kiasi cha Sh trilioni 1.7 kwa ajili ya kuiwezesha serikali kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuboresha mitaala katika mwaka wa fedha 2023/24.
Katika hotuba yake aliyoitoa bungeni, Dodoma leo asubuhi, Waziri amesema serikali imejipanga kukamilisha uandaaji wa mitaala itakayoendana na mahitaji ya sasa na kuwezesha wahitimu kuwa na ujuzi na maarifa stahiki.
Akitoa mchanganuo huo, Waziri ameliambia Bunge kuwa kati ya kiasi alichoomba kiidhinishwe, Sh bilioni 537.9 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida wakati Sh bilioni 500.957 zitatumika kwa ajili ya mishahara.
Aidha, kiasi cha Shilingi bilioni 36.9 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Alisema kuwa kiasi cha Shilingi trilioni 1.14 kinachoombwa kuidhinishwa ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo Shilingi bilioni 979.08 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 158.8 ni fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo.
Hata hivyo wabunge waliipongeza serikali kwa kuburesha miondombinu huku wakitaka kipaumbele kiwe kwenye elimu ya ufundi na kuongeza idadi ya walimu ili kukabiliana na upungufu.