Prof Mkumbo: Mamlaka za mitaa zivutie wawekezaji

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amezitaka mamlaka za serikali za mitaa kuwa sehemu ya kuvutia wawekezaji wa ndani na kuondoa vikwazo na kuwezesha shughuli za kiuchumi.

Waziri Mkumbo ametoa rai hiyo katika hafla ya uzinduzi wa eneo la starehe BRAVO COCOBEACH  lililopo eneo la Cocobeach Kinondoni, Dar es salaam lililobuniwa na kuhifadhiwa na mwekezaji wa ndani.

Advertisement

SOMA: Tanzania kuboresha mazingira ya uwekezaji

Pamoja na kukoshwa na ubunifu wa mazingira na utoaji huduma Prof Mkumbo amesema eneo hilo litumike kama mfano kwa wawekezaji wa ndani na halmashauri zingine ziige mfano wa Kinondoni.