Rais Ramaphosa atangaza Baraza la Mawaziri

PRETORIA, South Afrika – Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemteua kiongozi wa zamani wa upinzani John Steenhuisen kuwa waziri wa kilimo katika baraza la kwanza la mawaziri alilolitangaza jana usiku.

Baraza hilo pia limejumuisha wawakilishi wa vyama vya upinzani vinavyonda serikali ya Umoja wa Kitaifa kikiwemo chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance na vyama vingine.

Chama cha Ramaphosa cha African National Congress kililazimika kuunganisha nguvu na vyama hasimu ili kusalia madarakani baada ya kupoteza viti vya wabunge kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo mitatu katika uchaguzi wa Mei 29.


Tangazo la baraza jipya la mawaziri la serikali ya umoja wa kitaifa lilifuatia wiki za mazungumzo ya muda mrefu na wakati mwingine, uhasama.

Ramaphosa alibaki na Enoch Godongwana wa ANC kama waziri wa fedha huku Ronald Lamola akiteuliwa kuwa waziri wa uhusiano wa kimataifa na ushirikiano akichukua nafasi ya Naledi Pandor.

Gwede Mantashe alibakia kama waziri wa madini na petroli. Rais aliondoa sehemu ya nishati katika wizara hiyo.

SOMA: Treni ya Haraka kuanza safari za Dar – Moro

 

Habari Zifananazo

Back to top button