Rais Samia aanza ziara Afrika Kusini

RAIS wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewasili mji wa Pretoria kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya kiserikali nchini Afrika Kusini tarehe 15 Machi, 2023.
Rais Samia akishuka kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Waterkloof Air Force Base Pretoria.
Rais Samia akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Mtoto Malaika Adam Issara mara baada ya kuwasili Jijini Pretoria.
Rais Samia akiimba pamoja na baadhi ya Watanzania wanaoishi Pretoria nchini Afrika Kusini (Diaspora) mara baada ya kuwasili nchini humo tarehe 15 Machi, 2023