Rais Samia afanya uteuzi
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 9, 2023 amefanya uteuzi wa viongozi wawili.
Rais Samia amemteua Profesa Elifas Tozo Bisanda kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, Rais amemteua Mhandisi Abdallah Mohammed Mkufunzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Maji.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kwua uteuzi huo umeanza Mei 5, 2023.