Rais Samia akaribisha wawekezaji Hungary

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema amekubalina na Rais wa Hungary, Katalin Novak wawekezaji kutoka Hungary kuwekeza katika miradi ya kimkakati iliyopo hapa nchini.

Kiongozi huyo wa nchi amesema hayo leo Julai 18, 2023 Ikulu ya Magogoni Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mapokezi ya Rais Novak.

“Tumejadiliana juu ya wawekezaji kutoka Hungary kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya kimkakati kama vile nishati mbadala, uvivu utalii, madini na sekta za kifedha.” amesema Rais Samia.

Rais Samia amewataka viongozi katika sekta mbalimbali kuandaa mazingira rafiki pamoja na kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao watakapotaka kuwekeza nchini.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x