Rais Samia ampongeza Askofu Mteule Mihali

Askofu Mteule wa Jimbo Katoliki la Iringa, Padre Padre Romanus Elamu Mihali.

RAIS Samia Suluhu Hassan amempongeza Padre Romanus Elamu Mihali kwa kuteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Iringa Januari 28.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Fransisko amemteua Padre Mihali kuwa Askofu baada ya  kuridhia ombi la kustaafu Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo hilo.

Kupitia ukurasa rasmi wa X Rais Samia amesema: “Uteuzi wako ni ishara ya imani kubwa ya Kanisa kwa utumishi wako. Nakutakia kila la kheri. Mwenyezi Mungu akushike mkono, akubariki na kukuongoza, unapoendelea kushiriki kazi yake ya kuijenga jamii yetu kuwa bora zaidi katika jukumu hili jipya.”

Advertisement

Aidha Rais Samia amekariri maandiko ya Biblia katika kitabu cha Kutoka: 4:12 “Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.”

Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC), Padre Chesco Msaga imesema Mhashamu Askofu Mstaafu Ngalalekumtwa atakuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo la Iringa hadi Askofu Mteule Mihali atakapowekwa wakfu na kusimikwa jimboni humo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *