Rais Samia apokea taarifa kituo cha umeme Katavi

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Kituo cha kupokea na kupoza umeme wa Gridi ya Taifa kilichopo Inyonga Mkoani Katavi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga tarehe 13 Julai, 2024. Rais Dkt. Samia anaendelea na ziara yake ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi.(Picha: Ikulu Mawasiliano)