Rais Samia apongezwa kuwasikiliza wafanyabiashara

NAIBU Spika, Mussa Azzan Zungu amempongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kumuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufika viwanja vya Mnazi Mmoja kusikiliza kero za wafanyabiashara.

Pongezi hizo amezitoa leo wakati akizungumza katika mkutano wa Waziri Mkuu na wafanyabiashara wa soko la Kariakoo ambapo amesema kitendo cha Rais kumtuma Waziri Mkuu ni cha kupongeza na kuonesha utayari wa kutatua changamoto zao

Hata hivyo naibu spika amewaasa wafanyabiashara wa Kariakoo kufungua maduka yao

Advertisement

Itakumbukwa hii ni siku ya tatu ya mgomo wa wafanyabiashara hao unaochagizwa na wanachokieleza kuwa ni kero zilizokithiri

/* */