

RAIS Dk Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani.
Mjadala huo ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo.(Picha na Ikulu Mawasiliano)