Rais Samia ateua wenyeviti TRC, Veta

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Agosti 16, 2023 kutoka kitengo cha mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza Rais Samia amemteua Ally Amani Karavina kuwa Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania.

Aidha, Sifuni Ernest Mchome ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA )

Taarifa hiyo imeeleza uteuzi wa wenyeviti hao unaanza mara baada ya uteuzi huo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button