Rais Samia awaenzi mashujaa vita Maji Maji

RAIS Samia Suluhu Hassan ametembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji iliyopo Mjini Songea mkoani Ruvuma kwa lengo la kutoa heshima ya kumbukizi ya mashujaa wa vita ya Majimaji vilivyoanza mwaka 1905-1907.

Rais Samia amepokelewa na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii , wakiongozwa na  Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana, Katibu Mkuu,Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbasi, uongozi wa Mkoa wa Ruvuma , Chifu wa Wangoni Zulu Gama 1 , wazee wa mila na desturi Mkoa  wa Ruvuma na viongozi wa dini.

Advertisement

SOMA: Watanzania waadhimisha siku ya mashujaa

Pia Rais Samia ametembelea ukumbi wa historia ya vita ya Maji Maji, onesho la nyumba ya Inkosi ( Chifu) wa Kabila la Wangoni pamoja na shada la maua katika kaburi la halaiki la mashujaa wa vita ya Maji Maji  na kaburi la chifu msaidizi, Nduna Songea Luwafu  Mbano.

Aidha, Rais Samia ameweka silaha za jadi katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wa vita ya Kagera.