Rais Samia aweka shada la maua mnara wa uhuru Zambia

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa Uhuru wa Zambia.

Hatua hiyo ni ishara heshima na kutambua juhudi za waliogombania uhuru taifa hilo mwaka 1964.

Rais Samia pia ameweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa la Zambia, Dk Kenneth Kaunda jijini Lusaka.

Zambia inaadhimisha miaka 59 tangu ipate Uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1964.

Habari Zifananazo

Back to top button