Rais Samia azindua kampeni ya chanjo, utambuzi mifugo

BARIADI: RAIS Samia Suluhu Hassan amezindua kampeji ya kitaifa ya chanjo na utambuzi wa mifugo ambayo inatarajia kutekelezwa kwa miaka mitano inayogharimu Sh bilioni 216.
Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Nyakabindi Wilaya ya Bariadi mkoani Simyu na kampeini hiyo itatekelezwa kila mwaka kuanzia mwaka huu hadi 2029.
Kampeni hiyo ina lengo la kukidhi matakwa ya kimataifa ambayo inalitaka kila taifa linalohitaji kupeleka bidhaa ya nyama katika masoko ya nje ya nchi lazima mifugo yake iwe imechanjwa kwa asilimia 70.
SOMA ZAIDI
Zoezi la uzinduzi wa kampeini hiyo limeenda sambamba na Rais kugawa vifaaa vya kazi pikipiki kwa maafisa ugani na mifugo 700 ambapo amesema pikipiki hizo zifanye kazi iliyokusudiwa ya kuwasaidia wafugaji na sio shughuli nyingine za kibiashara.
Rais Samia pia ametoa vishikwanbi zaidi ya 4,000 kwa ajili ya kurahisisha usajili wa wafugaji kidigtali.