Rais Samia kuzindua soko la Kariakoo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua Soko la Kariakoo Februari 8, 2026, baada ya kukamilika kwa ukarabati wa soko la awali lililoungua kwa moto pamoja na ujenzi wa soko jipya.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema Soko la Kariakoo limekamilika kwa asilimia 100, huku zaidi ya Sh bilioni 28 zikitumika katika ukarabati na ujenzi wa soko jipya. Amesema soko hilo lina zaidi ya vizimba 1,500 vitakavyotumika na wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa, jambo litakaloongeza fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla.

Chalamila amewataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na wafanyabiashara wa makundi yote kujitokeza kwa wingi kushiriki uzinduzi huo, ili kumuunga mkono Rais Dk. Samia na kuweka historia ya tukio hilo muhimu la maendeleo.

Aidha, amewaagiza wafanyabiashara wadogo waliovamia na kufunga barabara zinazoingia katika Soko la Kariakoo kuondoka mara moja na kuziacha barabara hizo wazi kabla ya Februari 8, ili kuruhusu maandalizi ya uzinduzi kukamilika na wafanyabiashara kuanza kutumia soko hilo bila kikwazo. Uzinduzi wa Soko la Kariakoo unatarajiwa kuwa chachu muhimu ya biashara na maendeleo ya kiuchumi kwa Jiji la Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla. SOMA: Wafanyabiashara Soko la Kariakoo waandamana

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button