RC Mtaka atembelea TSN, ataja mikakati mipya

DAR ES SALAAM; Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, ametembelea Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) jijini Dar es Salaam kujadili ushirikiano wa kimawasiliano kuelekea Mei Mosi 2026.

Ziara hiyo inalenga kutumia vyombo vya habari kufikisha kwa umma fursa za kiuchumi zilizopo Njombe, hususan katika sekta za uchumi wa kijani kama parachichi, chai na misitu.

Mtaka amesema mkoa umebadili mkakati wa maadhimisho ya Mei Mosi kwa kuzingatia zaidi uhamasishaji wa uwekezaji na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo. Katika ziara hiyo Mtaka aliambatana na Katibu Tawala Mkoa, Dk.Stephen Nindi, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Dk Peter Maiga Nyanja na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Veronica Sanga.

Kupitia ushirikiano huo, TSN inatarajiwa kusaidia kuutangaza Mkoa wa Njombe kitaifa na kuvutia wawekezaji pamoja na kuongeza uelewa wa fursa zilizopo.



