RC Mtanda: lipeni bili za maji

MWANZA: MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ametoa wito kwa watumiaji wa huduma ya maji mkoani Mwanza pamoja na viunga vyake kutimiza wajibu wao kwa kulipia bili za maji kwa wakati pamoja na kulinda miundombinu ya maji.

Mtanda ameyasema hayo mara baada ya kufanya ukaguzi ili kujionea maendeleo ya mradi wa chanzo kipya cha maji uliopo Kata ya Butimba jijini Mwanza.

“Kuna haki na wajibu haki ya mteja ni kupata huduma ya maji na wajibu wa mteja ni pamoja na kulinda miundombinu ya maji na kulipa bili za maji kwa wakati,‚ÄĚamesema

” Mwauwasa inatumia gharama kubwa katika uendeshaji wa mitambo ya uzalishaji na usambazaji maji hivyo endapo wananchi wasipotimiza wajibu wao itasababisha Mwauwasa kushindwa kutoa huduma bora kutokana na kuzidiwa gharama za uendeshaji, amesisitiza

Katika hatua nyingine Mtanda amewasihi viongozi wa ngazi mbalimbali mkoani Mwanza kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya wajibu wao katika huduma ya maji ili kuiwezesha mamlaka kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Habari Zifananazo

Back to top button