RC Mtwara agawa vitanda kwa polisi wa Tangazo

MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amegawa vitanda 20 kwa kikosi cha Jeshi la Polisi kilichopo Tangazo Wilaya ya Mtwara.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vitanda hivyo, mkuu huyo wa mkoa wa Mtwara amesema askari hao na wanajeshi wengine muda mwingi wako kazini hawalali kuhakikisha mkoa huo uko salama.

Amesema kuna muda wanahitaji kupumzika ili wapate nguvu mpya kwahiyo vitanda hivyo vitawasaidia.

Advertisement

Hata hivyo anafahamu kuwa, vyombo hivyo vyote vina ushirikiano wa wenyewe kwa wenyewe, taasisi, wananchi katika kuhakikisha usalama wao unaendelea kuwa mzuri.

Amevipongeza vyombo hivyo kwa utendaji kazi wao na kama serikali imeahidi kuendelea kushikamana kama ilivyokuwa kawaida ili mkoa naTanzania kwa ujumla iendelee kuwa mahali salama.

‘’Kila mmoja mwenye nia njema na anayetamani kuja mtwara tunamkaribisha ikiwemo kuwekeza, kutalii, kufanya shughuli za kiuchumi na lingine lolote lile kwasababu vyombo vyetu hivi wanafanya kazi mzuri na wanatoa ushirikiana mkubwa na wanahakikisha mkoa wetu uko salama,’’amesema Sawala.

 

Aidha ameviomba vyombo hivyo kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa mkoa na nchi kwa ujumla izidi kuwa salama na amani ambayo imeachwa na waasisi wa nchi hiyo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleimani amemshukuru mkuu huyo ya mkoa kwa kutoa masaada huo wa vitanda kwa jeshi hilo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *