RC Mtwara awapa neno waandishi wa habari Mtwara

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya amewataka waandishi wa habari wilayani humo kuitendea haki taaluma yao kwa kufuata misingi ya uandishi katika kuhabarisha wananchi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu huyo wa Wilaya alipozungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya wa habari wilayani humo.

Amesema wanahabari ni nyenzo muhimu katika kutoa elimu na kuhamasisha wapiga kura hivyo ni vema kutumia weledi kuhabarisha ili kutimiza malengo yanayotarajiwa kwenye zoezi hilo.

Advertisement

“Hakikisheni mnalinda taaluma, maadili ikiwa ni pamoja na kufuata misingi ya uandishi kwa kuandaa habari zenye tija kuelekea zoezi hili,”amesema Nwaipaya.

Haya hivyo ni muhimu waandishi hao kuandaa vipindi vya maoni kwa ajili ya kupata maoni ya wananchi ili kuwahamasisha kujiandikisha na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Pia amewasihi viongozi wenzake kuwatumia vyema waandishi hao ili kuendelea kutangaza maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na hawawezi kufanikisha ajenda yeyote bila kushirikisha vyombo vya habari.

SOMA: Waandishi wa habari wafundwa

Ameongwza kuwa, “Kazi nyingi zinafanywa na Rais wetu lakini tusipowatumia vizuri waandishi wa habari hazitaonekana maana tukiviacha vyombo vya habari navyo vitatuacha”

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo, Mwalimu Hassan Nyange amesema jumla ya mitaa 111 inatarajiwa kushiriki uchaguzi huo.

Hata hivyo shughuli mbalimbali zimeshafanyika na zinaendelea kufanyika kuhamasisha wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu mchakato huo mzima wa uchaguzi.

SOMA: Waandishi wa habari wafundwa