Rose Ndauka awashukuru watanzania

TANGA: MSANII maarufu wa Bongo Fleva, Rose Ndauka, ametoa shukrani kwa mashabiki na Watanzania wote baada ya kuokolewa salama katika ajali ya gari alipokuwa njiani kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rose aliandika: “Ahsanteni sana wapenzi wangu kwa mapenzi yenu makubwa mliyonionyesha na mnayoendelea kunionyesha”.
Alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11:30 alfajiri, ambapo kwa bahati hakuna aliyepoteza maisha, ingawa wote walipata majeraha na wanaendelea kupokea matibabu. Msanii huyo pia alitoa taarifa ya kupotea kwa pochi yake nyeusi yenye mistari, iliyokuwa na pasipoti, pesa taslimu na simu ya aina ya iPhone 16, na aliweka namba ya mawasiliano kwa yeyote atakayepata pochi hiyo. SOMA: Watu saba wafa ajali ya gari Karagwe




