Mke wa Jota kumuenzi mumewe Jota
Rute aenzi kumbukumbu ya Jota

LISBON : MKE wa mshambuliaji wa Liverpool, Diogo Jota, Rute Cardoso, ameadhimisha mwezi mmoja tangu kufunga ndoa na mchezaji huyo, wiki tatu baada ya kufariki dunia katika ajali ya gari.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rute alipakia picha tatu za harusi yao iliyofanyika Juni 22, na kuandika “Mwezi mmoja wa ahadi yetu kifo kitakapotutenganisha , ni wangu milele ,” alisema. SOMA: Diogo Jota afariki kwa ajali
Jota (28) alifariki Julai 3 baada ya gari aina ya Lamborghini alilokuwa akisafiria pamoja na mdogo wake, Andre Silva, kupoteza mwelekeo, kupinduka na kushika moto katika eneo la Cernadilla, jimbo la Zamora, nchini Uhispania.




