Rwepas sekondari wajiweka sawa maadili

WAZAZI wanaosomesha watoto wao katika shule ya Sekondari Rwepas iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwachunga watoto wao kwa kuepuka kuwapatia simu hasa wanapomaliza kidato cha nne.

Mwalimu mstaafu Catherine Kisula amesema hayo wakati wa sherehe ya mahafali ya shule ya Sekondari Rwepas iliyopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Kisula amesema dunia ya sasa imeharibika kwa baadhi ya watu kufuata baadhi ya mambo kwenye mitandao yasiyo na maadili hivyo wazazi wanatakiwa kuwa makini pindi watoto wanapokuwa na simu zao.

“Vipo vitendo vya ubakaji,ulawiti na usagaji ambapo mtatoka hapa mkiwa na maadili mazuri hivyo msiende kuyafuata mambo hayo ambayo kinyume na maadili,”amesema Kisula.

SOMA: Samia asisitiza maadili bora kwa watoto

Kisula amesema zipo jitihada zilizofanyika kuinyanyua shule hii kufikia kiwango kizuri cha ufaulu na wanafunzi wanaohitimu mwaka huu wasiiangushe shule kupata daraja la nne au sifuri.

Meneja wa shule hiyo, Frank Samweli amesema shule hiyo imeweka kipaumbele cha kwanza ni maadili na taaluma kwa mwanafunzi na mpaka sasa kuna wanafunzi 380 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na walimu 22.

SOMA: Samia: Tuangalie tulipojikwaa mmomonyoko wa maadili

“Wahitimu wa kidato cha nne wako 58 lakini walianza kidato cha kwanza wakiwa wanafunzi 25 mwaka 2021 lakini sasa maboresho makubwa yamefanyika ya kunyanyua kiwango cha taaluma kwa kushirikiana na wazazi,” amesema Samweli.

Samweli amesema maboresho makubwa yamefanyika kuna maabara ya masomo ya sayansi na komputa wanafunzi wamekuwa wakijifunza kwa vitendo.

Kwa niaba ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne Ghati Charles akisoma risala amesema watatekeleza yote wanayoelezwa nakuwataka wazazi waendelee kutoa ushirikiano kwa walimu.

Habari Zifananazo

Back to top button